⚖️ VIASHIRIA VYA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU — TOA TAARIFA!
🚨 Usafirishaji haramu wa binadamu unaweza kutokea katika mazingira ya kazi za ndani (viwandani, mashambani n.k) katika ajira, safari au mahusiano. Wakati mwingine, wahanga huishi karibu nasi bila sisi kutambua wanachopitia.
🔎 ZINGATIA VIASHIRIA HIVI:
Kunyimwa uhuru: Mtu anazuiwa kuondoka kazini au mahali anapoishi, au anafuatiliwa kila anapotaka kutoka.
Majeraha au vidonda: Mtu ana majeraha mwilini kuashiria kipigo kutoka kwa mtu anayemmiliki.
Uoga au unyenyekevu uliopitiliza: Waathirika wengi wa Usafirishaji haramu wa binadamu wanakuwa waoga sana kutokana na vitendo vya ukatili wanavyopitia.
Kuchukuliwa nyaraka: Pasipoti, kitambulisho au nyaraka nyingine zinashikiliwa ili kumdhibiti.
Kazi za kulazimishwa: Mtu analazimishwa kufanya kazi kwa vitisho, bila malipo yanayostahili au katika mazingira ya unyonyaji na kufanya kazi kwa muda mrefu sana bila mapumziko.
Malipo ya kazi anazofanya anapokea mtu mwingine. Huu ni unyonyaji pia, mtu anapofanya kazi anastahili kulipwa kutokana na jasho lake lakini si mtu mwingine kupokea fedha ambazo hakuzifanyia kazi.
Vitisho na udhibiti: Mtu anatishwa, anapigwa au anakaripiwa mara kwa mara na kuadhibiwa hata kwa makosa madogo madogo.
Ahadi za uongo: Mtu anashawishiwa kwa ahadi za ajira, ndoa au maisha bora, kisha anajikuta akinyonywa.
Kunyimwa mawasiliano: Mtu haruhusiwi kuwasiliana kwa uhuru na familia au watu wengine.
⚠️ Kumbuka: Kiashiria kimoja pekee hakithibitishi kuwa kosa la usafirishaji haramu wa binadamu limetendeka. Hata hivyo, mazingira yanayotia shaka yanastahili kuchukuliwa kwa uzito.
📢 UNA TAARIFA AU UNASHUHUDIA HALI INAYOTIA SHAKA? TOA TAARIFA!
Tuma ujumbe wa faragha kwa Jungu La Sheria kupitia WhatsApp au piga simu +255 628 729 934 ili kupata mwongozo kuhusu hatua zinazofaa kuchukuliwa na namna ya kufikisha taarifa kwa mamlaka husika.
🛡️ Usikae kimya. Taarifa yako inaweza kusaidia kumlinda mhanga na kuzuia unyonyaji zaidi.
Jungu La Sheria — Sheria | Tehama

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿