Kwa MUJIBU wa sheria ya ndoa kifungu 161, endapo mwanandoa mmoja atapoteza mawasiliano na mwanandoa mwenzie kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo bila ya taarifa au mawasiliano yoyote na bila kujua mwenzi wake yupo wapi. Sheria inatambua hali hiyo kama dhana ya kifo hivyo Sheria itachukulia kuwa mtu huyo amefariki na mwenzi wake anaweza kuomba mahakama itoe amri ya kuvunja ndoa yao na anaweza kuolewa Tena na mtu mwingine.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿