Ticker

6/recent/ticker-posts

KUTOHUDHURIA KWA MLALAMIKAJI SIKU YA KUSIKILIZA KESI.



SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI SURA YA 20 ILIYOREJEWA MWAKA 2019.

KIFUNGU CHA 222 KINASEMA,

Iwapo, katika kesi yoyote ambayo  mahakama ya chini ina mamlaka  kusikiliza na kuamua, mtuhumiwa amehudhuria kwa kutii wito aliopelekewa katika muda na mahali palipoteuliwa katika wito kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi,  au ameletwa mbele ya mahakama akiwa amekamatwa, kwa hiyo, kama mlalamikaji, baada ya kupewa taarifa ya muda na mahali palipoteuliwa  kwa ajili ya kusikiliza shitaka hatahudhuria, mahakama italazimika kutupilia mbali shitaka na kumwachia huru mtuhumiwa, isipokuwa kama  kwa sababu fulani, italazimika  kufikiri ni vema kuahirisha usikilizaji, wa kesi mpaka tarehe nyingine na, wakati akisubiri usikilizaji ulioahirishwa, ama kumuachia mtuhumiwa kwa  dhamana au kumweka rumande  au kuchukua dhamana kwa ajili ya kuhudhuria kwake kama mahakama itakavyoona inafaa.

Imeandikwa na Mwanasheria

Johnson Yesaya Mgelwa

Wa Jungu la sheria Tanzania

0758218269/0628729934


Chapisha Maoni

0 Maoni