🇹🇿 Je, Rais anaweza kukamatwa au kulazimishwa kufika mahakamani?
📜 Kwa mujibu wa Kifungu cha 9 cha Sheria ya Masuala ya Ofisi ya Rais.
• Rais ana kinga dhidi ya kukamatwa.
• Hakuna mahakama au mamlaka yenye uwezo wa kutoa hati inayoweza kumlazimisha Rais kufika au kuhudhuria kwa namna yoyote vikao vya mahakama, au kumlazimisha kuwasilisha mtu au kitu.
• Hata hivyo, ikiwa mtu anaomba Rais aitwe kama shahidi au awasilishe mtu au kitu, mahakama inaweza kumjulisha Rais kuhusu ombi hilo, lakini haiwezi kutoa amri nyingine au hati ya kumlazimisha kwa msingi wa ombi hilo.
#JunguLaSheria ⚖️
#ElimuYaSheria 📚
#TanzaniaLaw 🇹🇿
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿