Ticker

6/recent/ticker-posts

Kuruhusu Uchangudoa kwenye eneo lako ni kosa la jinai.



Mtu yeyote ambaye, akiwa muangalizi wa baa, hoteli, nyumba, duka, chumba au mahali pengine popote pa burudani kwa ajili ya kuuza au kutumia vinywaji vya aina yoyote, kwa kujua, anamruhusu au kuvumilia makahaba kukusanyika na kubaki katika eneo lake kwa ajili ya ukahaba, atakuwa na hatia na atawajibika kwa adhabu ya faini isiyozidi shilingi elfu hamsini au, kwa kosa la pili au la baadae, faini isiyozidi shilingi laki tano.


Kifungu 176A kanuni ya adhabu sura ya 16.

Chapisha Maoni

0 Maoni