Kwa mujibu wa kifungu cha 217 cha kanuni ya adhabu sura ya
16, kujaribu kujiua ni kosa la jinai. Kosa hilo linaweza kuhukumiwa kwa adhabu
isiyozidi miaka 5 jela kama inavyoelekezwa na kifungu cha 35 kinachoeleza
adhabu ya jumla kwa makosa ambayo hayajapewa adhabu ya moja kwa moja.
Lakini sheria hiyohiyo inaweka kinga katika kifungu cha 13 na
inatoa msamaha kwa watu wanaofanya makosa wakiwa katika hali ya ugonjwa unaoathiri
akili zao na kufanya wasielewe wanachofanya.
Hivyo basi, endapo mtu amejaribu kujiua akiwa na akili timamu
na ikathibitika hivyo, atahukumiwa kwa adhabu isiyozidi miaka 5, lakini kama amejaribu
kujiua akiwa na hali ya ugonjwa unaoathiri akili yake na kufanya kosa bila kuelewa,
hatakuwa na kosa kisheria kwa kuwa sheria inampa kinga.
Endapo mtu huyo amefikishwa mahakamani, na ikabainika alifanya
kosa akiwa katika hali ya ugonjwa, Basi mtu huyo hana hatia, mahakama inaweza kuamua
mtu huyo kupelekwa katika kituo cha uangalizi wa watu wenye changamoto ya afya ya
akili kwa mujibu wa kifungu cha 219(2)(b) Cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai
sura namba 20.
⚖️ Tatizo Lako la Kisheria Linahitaji Majibu Sahihi?
Elimu ya sheria inayotolewa kwenye makala hii ni ya jumla. Ikiwa unahitaji ufafanuzi kuhusu hali yako binafsi, unaweza kuongea moja kwa moja na Mwanasheria na kupata ushauri unaoendana na mazingira yako.
✅ Utakachopata
✔️ Uchambuzi wa suala lako la kisheria
✔️ Majibu ya maswali yako moja kwa moja
✔️ Mwongozo wa hatua za kuchukua
✔️ Ushauri wa kitaalamu unaozingatia mazingira yako
✔️ Usiri wa kitaalamu katika mawasiliano yote
📚 Maeneo Tunayotoa Ushauri
Ardhi • Mirathi • Ndoa na Talaka • Ajira • Mikataba • Madeni • Biashara • Mashauri ya Madai • Mashauri ya Jinai na masuala mengine ya kisheria.
💰 Ada ya Ushauri: TSh 30,000 Tu
📲 Fanya Malipo Kupitia Mojawapo ya Njia Zifuatazo
✅ Airtel Money LIPA: 13970429
✅ Yas/Tigo LIPA: 18401500
✅ M-Pesa Wakala: 826910
✅ Selcom Lipa: 61122934
✅ CRDB Lipa TANQR: 11692089
Jina la Mpokeaji:
Johnson Yesaya Mgelwa
📩 Baada ya Kufanya Malipo
Tuma ujumbe mfupi wa kuthibitisha malipo yako kupitia WhatsApp au SMS. Utapigiwa simu ndani ya dakika 10 kwa ushauri wa kisheria.
💬 TUMA UTHIBITISHO WA MALIPO+255 628 729 934

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿