Tume ya Uchunguzi nchini Tanzania ni chombo cha kisheria kinachoanzishwa chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32 [R.E 2002]. Kifungu hiki kinampa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mamlaka ya kuunda tume ya kuchunguza masuala mbambali yenye maslahi ya umma. Uanzishaji wa tume hii unaweza kufanywa na Rais mwenyewe, kwa kushauriana na Waziri, au baada ya kuchunguza taarifa zilizowasilishwa kwa kiapo na mtu yeyote. Madhumuni makuu ni kushughulikia masuala yanayoathiri ustawi wa umma, kuhakikisha uwajibikaji na uwazi katika shughuli za serikali au maeneo mengine yenye maslahi ya umma.
Tume ya Uchunguzi kwa kawaida huanzishwa kuchunguza mambo mbalimbali kama yenye maslahi ya umma kama mienendo ya watumishi wa umma, mamlaka za mitaa, idara za huduma za umma, ukwepaji kodi, upungufu katika mapato ya umma, rushwa, na ulanguzi wa rasilimali asilia. Rais ana uwezo wa kuamua wigo wa uchunguzi, kuteua makamishna, na kuamua muda na mahali ambapo uchunguzi utafanyika. Tume inaweza kufanya shughuli zake hadharani au faraghani, kulingana na maelekezo ya Rais.
Tume hutekeleza jukumu lake kwa kuchunguza na kuripoti kwa Rais matokeo ya uchunguzi na mapendekezo ya hatua za kuchukua. Makamishna wana mamlaka ya kuita mashahidi, kupitia nyaraka, na kuchukua ushahidi chini ya kiapo, sawa na nguvu zinazotumiwa na Mahakama Kuu. Uchunguzi huu ni wa kisheria, na unaruhusu makamishna kutumia huduma za wataalamu pale inapohitajika.
Uteuzi wa makamishna, majukumu yao, na kanuni zinazoongoza uchunguzi zimewekwa wazi katika sheria tajwa hapo juu. Makamishna wanatakiwa kuapa kiapo cha uaminifu na kufanya uchunguzi huo kwa haki. Sheria pia inaeleza taratibu za kuitisha mashahidi, kupokea ushahidi, na kutoa ripoti. Aidha, sheria inatoa kinga dhidi ya mashtaka kwa makamishna na maafisa wengine wanaoshiriki katika uchunguzi.
Iwapo kamishna hawezi kuendelea na majukumu yake, Rais ana mamlaka ya kuteua mbadala wake, na tume yoyote inaweza kubadilishwa au kufutwa na Rais wakati wowote. Matokeo ya uchunguzi yanaweza kupelekea mashtaka, au hatua nyingine za kiserikali kulingana na maamuzi ya Rais.
Kupitia tume hizi, serikali ya Tanzania inahakikisha kuwa masuala ya maslahi ya umma, hasa yale yanayohusisha mwenendo mbovu au ukiukwaji wa sheria, yanachunguzwa kikamilifu na hatua stahiki zinachukuliwa ili kulinda ustawi wa umma na kudumisha utawala wa sheria.
⚖️ Tatizo Lako la Kisheria Linahitaji Majibu Sahihi?
Elimu ya sheria inayotolewa kwenye makala hii ni ya jumla. Ikiwa unahitaji ufafanuzi kuhusu hali yako binafsi, unaweza kuongea moja kwa moja na Mwanasheria na kupata ushauri unaoendana na mazingira yako.
✅ Utakachopata
✔️ Uchambuzi wa suala lako la kisheria
✔️ Majibu ya maswali yako moja kwa moja
✔️ Mwongozo wa hatua za kuchukua
✔️ Ushauri wa kitaalamu unaozingatia mazingira yako
✔️ Usiri wa kitaalamu katika mawasiliano yote
📚 Maeneo Tunayotoa Ushauri
Ardhi • Mirathi • Ndoa na Talaka • Ajira • Mikataba • Madeni • Biashara • Mashauri ya Madai • Mashauri ya Jinai na masuala mengine ya kisheria.
💰 Ada ya Ushauri: TSh 30,000 Tu
📲 Fanya Malipo Kupitia Mojawapo ya Njia Zifuatazo
✅ Airtel Money LIPA: 13970429
✅ Yas/Tigo LIPA: 18401500
✅ M-Pesa Wakala: 826910
✅ Selcom Lipa: 61122934
✅ CRDB Lipa TANQR: 11692089
Jina la Mpokeaji:
Johnson Yesaya Mgelwa
📩 Baada ya Kufanya Malipo
Tuma ujumbe mfupi wa kuthibitisha malipo yako kupitia WhatsApp au SMS. Utapigiwa simu ndani ya dakika 10 kwa ushauri wa kisheria.
💬 TUMA UTHIBITISHO WA MALIPO
+255 628 729 934
Usifanye Maamuzi ya Kisheria Bila Ushauri wa Kitaalamu.
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿